IQNA

Warsha ya ‘Uhusiano na Qur’ani’ katika shule 120,000 Iran

12:07 - May 12, 2011
Habari ID: 2120851
Mshauri wa masuala ya Qur’ani katika Wizara ya Elimu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa warsha zenye anwani ya ‘Uhusiano na Qur’ani’ zitafanyika katika sule 120,000 kote nchini.
Mohammad Bonyadi ambaye ni mkurugenzi mkuu wa Idara ya Qur'ani na Sala katika Wizara ya Elimu amemuambia mwandishi wa IQNA kuwa warsha hizo zitaanza mwaka mpya wa kiakademia ambao kwa kawaida huanza mwezi Septemba nchini Iran.
Amesema shule zote za msingi na sekondari zimeshurutishwa kuandaa warsha hizo pamoja na mashindano wa Qur’ani na Sala katika mwaka mpya wa kiakademia.
Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu, warsha hizo zitajumuisha mada kama vile hotuba za Qur’ani, hadithi za Qur’ani, tafsiri na tarjumi ya Qur’ani, mashairi ya Qur’ani n.k.
789824



captcha