IQNA

Mauaji ya wananchi wa Bahrain yalaaniwa katika Sala ya Ijumaa Tehran

11:58 - May 14, 2011
Habari ID: 2121359
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa jana mjini Tehran, amelaani vikali mauaji yanayofanywa na vibaraka wa utawala wa Kifalme wa Aal- Khalifa na Aal Saudi nchini Bahrain dhidi ya wananchi wa nchi hiyo wasio na hatia.
Ayatullah Ahmad Jannati amesema hayo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya kisiasa na kimaanawi ya Sala ya Ijumaa na kubainisha kwamba, serikali ya Saudi Arabia imekuwa ikiisadia Bahrain kifedha, kisiasa na kijeshi katika kuwauwa wananchi wa Bahrain wanaoandamana wakitaka mabadiliko ya mfumo wa kisiasa katika nchi hiyo.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran ameashiria uadui unaofanywa dhidi ya taifa la Iran na kutanabahisha kwamba, vikwazo dhidi ya Tehran vimekuwa chachu ya mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyuga zote.
Aidha Ayatullah Jannati ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Kulinda Katiba hapa nchini, amesisitiza juu ya nafasi muhimu ya Wilayatul Faqih yaani Utawala wa Fakihi na kubainisha kwamba, Utawala wa Fakihi ni nguzo ya mfumo mtukufu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
790901
captcha