IQNA

Kongamano la ‘Miujiza ya Kisayansi katika Qur’ani’ kufanyika Uturuki

12:43 - May 14, 2011
Habari ID: 2121360
Kongamano la Pili la Kimataifa la Miujiza ya Kisayansi katika Qur’ani Tukufu’ linaanza leo Mei 14 katika Taasisi ya Utamaduni ya Forat mjini Istanbul nchini Uturuki.
Kwa mujibu wa tovuti ya Turkia al Yawm, kongamano hilo linafanyika kwa ushirikiano wa majarida ya Hera, Sizinti na Yeni Umit ya Uturuki.
Kongamano hilo la siku mbili litahudhuriwa na wasomi na wataalamu kutoka Uturuki na nchi kadhaa duniani.
Uchunguzi kuhusu sayansi za kisasa na miujiza ya Qur’ani ni kati ya mada zitakazojadiliwa katika vikao saba vya kongamano hilo.
Washiriki wa kongamano hilo ni pamoja na Abdullah bin Abdulaziz Al-Muslih, Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Miujiza ya Qur’ani na Mohammad Ali Al-Bar wa Saudi Arabia , Hassan Shamsi Basha wa Syria, Husna Hamdan wa Misri Egypt na Ghamaruddin bin Mohammad Yusuf wa Malaysia .
790868
captcha