Amesema ulimwengu wa Kiislamu unashuhudia mabadiliko ambayo yanahitajia hekima na busara katika kuyashughulikia. Ameashiria matukio yanayokwenda kwa kasi katika baadhi nchi za OIC na kusisitiza ulazima wa kuharakisha utekelezwaji wa matakwa ya wananchi kama vile utawala bora, utawala wa sheria, uzingatiwaji haki za binaadamu na kupanuliwa uwanja wa kisiasa na mazungumzo ya kitaifa kwa msingi wa ikhlasi.
Ihsanoglu ameyasema hayo Mei 15 mjini Jeddah alipofungua mkutano wa siku tatu wa maafisa wa ngazi za juu wa kutayarisha kikao cha 38 cha Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa OIC.
Kuhusu kadhia ya Palestina Katibu Mkuu wa OIC amesema vitendo vilivyo kinyume cha sheria vya utawala haramu wa Israel vinaibua masali mazito kuhusu hatima ya Quds Tukufu. Ihsanoglu ameashiria njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kuharibi muundo wa Kiarabu na Kiislamu wa Baitul Muqaddas na kusema vitendo hivyo vya Wazayuni ni vita vya wazi dhidi ya Wapalestina na Ulimwengu wa Kiislamu.
Ameelezea matumaini yake kuwa mkataba wa umoja wa kitaifa Palestina kati ya Hamas na Fat'h utaweza kuwaunganisha Wapalestina ili waweza kukabiliana na changamoto zilizopo.
Ihsanoglu pia ametoa wito kwa nchi za Kiislamu na jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kivitendo za kuunda taifa huru la Palestina, Quds Tukufu ikiwa mji wake mkuu.
792609