IQNA

Kituo cha Qur'ani cha Bibi Fatima (as) chafunguliwa Jordan

19:22 - May 16, 2011
Habari ID: 2123337
Kituo cha Qur'ani cha Bibi Fatima (as) kimefunguliwa katika mkoa wa al Aqaba nchini Jordan kwa hima ya Jumuiya ya Kulinda Qur'ani Tukufu.
Kituo hicho kimefunguliwa katika sherehe iliyohudhuriwa na Nidhal al Ibadi ambaye ni mjumbe wa Baraza la Idara ya Jumuiya ya Kulinda Qur'ani Tukufu.
Mkuu wa jumuiya hiyo katika eneo la al Aqaba Umar Said amewashukuru watu waliojitolea kujenga kituo hicho cha Qur'ani na kupongeza jumuiya yake kwa kutoa huduma nzuri za Qur'ani.
Amesema Jumuiya ya Kulinda Qur'ani ya Jordan imetoa huduma kubwa katika masuala ya Qur'ani ikiwa ni pamoja na kuanzisha vituo 800 vya Qur'ani nchini Jordan, kutoa elimu na mafunzo ya Qur'ani kwa wanafunzi 8 waliohitimu masomo na makarii 100, kuwa na wanachama 25 elfu ambao ni wanafunzi, kuchapisha nakala elfu 7 za jarida la al Furqan na tasiri ya Qur'ani kwa lugha ya ishara. 792467


captcha