IQNA

Kongamano la Utafiti wa Qur'ani na afya kufanyika Iran

19:24 - May 17, 2011
Habari ID: 2123810
Kongamano la kwanza la 'Utafiti wa Qur'ani na afya litafanyika Isfahan nchini Iran Mei 18.
Kongamano hilo limeandaliwa na Kitengo cha Mafunzo ya Kiislamu na litajadili mbinu za utafiti wa Qur'ani na masuala ya afya na vilevile mtazamo wa Qur'ani kuhusu mwanadamu.
Ali Gholami Dehaghi katibu wa kongamano hilo amesema utafiti wa Qur'ani unalenga kufahamu zaidi hekima ya Qur'ani.
Amesema kuwa mtazamo wa Qur'ani kuhusu maadili ya kikazi kwa wanaofanya kazi katika sekta ya afya, mafundisho ya Qur'ani na afya ya kisaikolojia, uhusiano baina ya sayansi na dini kwa kuzingatia Qur'ani na afya, mfumo wa afya kwa mtazamo wa Qur'ani na mtazamo wa Qur'ani kuhusu uadilifu katika afya ni kati ya mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo la siku mbili.
793224
captcha