IQNA

Mashindano ya Qur'ani kufanyika Massachusetts Marekani

15:03 - May 18, 2011
Habari ID: 2124653
Mashindano ya kosoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu yamepangwa kufanyika miezi miwili ijayo katika mji wa Springfield katika jimbo la Massachusetts huko Marekani.
Lengo la mashindano hayo ambayo yanasimamiwa na Kituo cha Kiislamu cha Massachusetts limetajwa kuwa ni kuwahimiza watu kusoma, kuhifadhi na kutaamali kitabu kitakatifu cha Qur'ani. Mashindano hayo yatakuwa yakifanyika mara moja kila baada ya miezi minne.
Katika upande wa Qiraa, duru hii ya mashindano ya Qur'ani itakuwa na sehemu 4 za kusoma sura za kuanzia 96 hadi 114 za Qur'ani kwa watoto wenye umri wa miaka 7 na 8, kusoma juzuu ya 28 hadi 30 kwa watoto wenye umri wa miaka 9 hadi 12, kusoma juzuu 10 na juzuu tano za mwisho za Qur'ani kwa watu wenye umri wa juu ya miaka 13.
katika upande wa hifdhi ya Qur'ani, kutakuwepo sehemu kadhaa ikiwa ni pamoja na hifdhi ya sura za kuanzia 110 hadi 114 kwa watoto wenye umri wa miaka 5 na 6, kuhifadhi sura za 99 hadi 114 za Qur'ani kwa watoto wenye umri wa miaka 7 na 8, kuhifadhi juzuu ya 30 makhsusi kwa watoto wenye umri wa miaka 9 hadi 12 na kuhifadhi juzuu mbili za mwisho kwa watoto wenye umri wa miaka 13 na kuendelea.
Washindi wa mashindano hayo watatunukiwa zawadi nono. 793442

captcha