Kwa mujibu wa gazeti la Dar al-Hayat la Saudia, OIC imetoa taarifa ikiwasilisha pendekezo la kubadilishwa jina na kaulimbiu ya jumuiya hiyo, jambo ambalo litajadiliwa katika kikao cha mwishoni mwa mwezi Juni cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo huko Kazakhstan.
Lengo la kutolewa pendekezo hilo limetajwa kuwa ni kwenda sambamba na matukio ya hivi karibuni katika ulimwengu wa Kiislamu na kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya nchi wanachama.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha kuaminika jina la jumuiya hiyo huenda likabadilishwa na kuwa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu. Jina hilo limechaguliwa kati ya majina mengine kama vile Umoja na Mshikamano wa Kiislamu. Nembo mpya ya jumuiya hiyo imependekezwa iwe ni al-Kaaba Tukufu, na nara yake kusisitiza juu ya uwastani katika mafundisho ya Kiislamu. 795091