Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe za kufunga mashindano hayo zilianza kwa kisomo cha Qur’ani Tukufu na kufuatiwa na qasida.
Akihutubu katika hafla hiyo, kamanda wa Jeshi la Pilisi la Iran Mostafa Ahmadi Moqqadam amesema, ‘Qur’ani ni kitabu cha shafaa kwa wanadamu wote. Iwapo mwanadamu atatambua adhama ya Qur’ani basi atagundia kuwa kitabu hicho kitakatifu ndio njia bora zaidi ya kuongoza umma ili kufukia ukamilifu’.
Ameongeza kuwa iwapo mwanadamu ataacha kutekeleza hata muongozo mmoja wa Qur'ani atakabiliwa na matatizo katika maisha yake.
Mashindano ya 28 ya Qur’ani Tukufu ya Vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalifanyika tarehe 17 na 18 Mei ambapo kulikuwa na washiriki 233 katika vitengo vya qiraa, hifdhi,, tartil, utafiti na tafsiri, adhana na hadithi. Mashindano hayo yalifanyika katika makao ya Vikosi vya Jeshi la Polisi mjini Tehran.
794302