IQNA

Misikiti sita mipya kujengwa katika mji mkuu wa Sweden

10:36 - May 22, 2011
Habari ID: 2126203
Misikiti sita mipya itajengwa katika mji mkuu wa Sweden, Stockholm ambao kwa sasa una misikiti miwili tu.
Kituo cha Islam Today kimeripoti kuwa uamuzi huo wa kujenga misikiti mipya sita katika mji wa Stockholm umechukuliwa kutokana na uhaba wa misikiti katika mji huo.
Mitatu kati ya misikiti hiyo sita itajengwa ndani ya mji wa Stockholm na mingine mitatu itajengwa katika viunga vya mji huo.
Makundi mbalimbali ya Waislamu yanaishi katika mji wa Stockholm na yanahitaji misikiti kwa ajili ya kutekeleza ibada zao za kidini.
Mpango wa kujengwa msikiti wa kwanza kabisa katika jiji la Stockholm ulipasishwa na baraza la mji huo mwaka 1995 baada ya juhudi za miaka 20 za Waislamu wa Sweden na ujenzi wake ulikamilika mwaka 2000. 795594
captcha