Ikitoa taarifa kuhusiana na suala hilo halmashauri hiyo imesema kuwa kufuatia matamshi ya hivi karibuni ya Ahmad Tayyib Sheikh wa al-Azhar kuhusiana na udharura wa kuanzishwa tena mazungumzo hayo, hivi karibuni Nabil al-Arabi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri aliwakabidhi wakuu wa Vatican barua ya kutangaza msimamo wa al-Azhar kuhusu jambo hilo. Taarifa hiyo imesema kuwa Sheikh wa al-Azhar ameelezea matumaini yake ya kuondolewa matatizo yaliyopo kati ya kituo hicho muhimu cha Kiislamu na Vatican ikiwa ni katika juhudi za kuandaliwa mazingira ya kuhuishwa mazungumzo hayo.
Tunakumbusha hapa kwamba mazungumzo ya kidini kati ya vituo viwili hivyo muhimu vya kidini yalisimamishwa mwanzoni mwa mwaka huu kufuatia matamshi ya kashfa ya Papa Benedict XVI kuhusiana na hali ya Wakristo nchini Misri. 796752