IQNA

Qur'ani kuwekwa katika vyumba vya hoteli Imarati

22:53 - May 23, 2011
Habari ID: 2127295
Hoteli katika Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) zinaweza kuweka Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiarabu na lugha nyinginezo katika vyumba maadamu misahafu hiyo inaheshimiwa.
Hayo ni kwa mujibu wa idhini iliyotolewa na Kituo cha Fatuwa cha Wizara ya Uadilifu cha Imarati kufuatia swali lililoulizwa iwapo inajuzu kuweka Qur'ani Tukufu katika vyumba vya hoteli hasa kwa kuzingatia kuwa baadhi ya wateja si Waislamu.
"Kuweka Qur'ani katika vyumba vya hoteli ni jambo linalojuzu maadamu heshima yake inadumishwa", imesema fatuwa iliyochapishwa na gazeti la kila siku la Al Khaleej.
Fatuwa hiyo imeongeza kuwa, 'Hoteli pia zinaweza kuweka Qur'ani kwa lugha nyinginezo vyumbani kwani zinaweza kuguswa na wengine na maadamu zinaheshimiwa'.
797130

captcha