Kongamano hilo linasimamiwa na ofisi ya kiutamaduni ya Baraza Kuu la Masuala ya Familia la Sharja likishirikiana na Benki ya Kiislamu na taasisi ya Marami.
Mtafiti wa masuala ya Qur’ani wa Imarati Sabri al Damardash atahutubia kongamano hilo kuhusu ‘udharura wa kutiliwa maanani muujiza wa kisayansi wa Qur’ani’.
Wasomi wengine watakaohutubia kongamano hilo ni Ustadh Hamid al Nuaimi ambaye anazungumzia ‘siri za dunia katika aya za Qur’ani’ na Khalid al Ubaidi ambaye atazungumzia ‘mfumo wa kiuhandishi katika Qur’ani Tukufu’.
Wasomi wengine wa Kiislamu pia wamewasilisha makala kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na muujiza wa Qur’ani Tukufu. 797437