IQNA

Siasa mpya za Misri kuimarisha uhusiano na Iran

12:15 - May 25, 2011
Habari ID: 2128318
Kamal Ahmed al- Janzuri, Waziri Mkuu wa zamani wa Misri amesema kuwa siasa mpya za nje za nchi hiyo zitaimarisha uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akizungumzia suala hilo huko Cairo hapo siku ya Jumatatu katika Kikao cha Mazungumzo ya Kitaifa, al-Janzuri, amesema kuwa siasa mpya za Misri zinaunga mkono moja kwa moja suala la Palestina na kuwa na uhusiano wa karibu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amesema hata kama udiplomasia wa Misri ulikuwa sawa na wa Ulaya kuhusiana na kadhia ya Palestina lakini siasa za nje za nchi hiyo zilisimama juu ya msingi wa mtazamo wa kidikteta wa mtu mmoja na hivyo kutotilia maanani matakwa ya wananchi wa Misri. Akisema kuwa ulimwengu unaendeshwa na mfumo wa kiuchumi, al-Janzuri amesisitiza kwamba kwa kutoa madai ya uongo ya eti kupambana na ugaidi na kuziletelea demokrasia nchi za Mashariki ya Kati, Marekani imeanzisha vita vikubwa katika eneo hilo kwa lengo la kupora mali na utajiri wa mataifa ya Kiislamu ya eneo hili muhimu. Amesema kwa msingi huo vita hivyo vinapaswa kutajwa kuwa vya kiuchumi na wala sio vya kupigania demokrasia.
Wakati wa uwaziri mkuu wake al-Janzuri alipendwa sana na Wamisri kutokana na misimamo yake ya kisiasa, jambo lililompelekea dikteta Hosni Mubarak kumuuzulu. 797811
captcha