IQNA

Mashindano ya Kimataifa Iran kuanza 27 Rajab (Juni 30)

21:50 - May 25, 2011
Habari ID: 2128620
Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yanatazamiwa kuanza Juni 30 itakayosadifiana na tarehe 28 Rajab mwaka huu sambamba na mnasaba wa kubaathiwa Mtume Muhammad SAW.
Mashindano hayo ya Qur'ani ambayo huandaliwa na Shirika la Awqaf la Iran yatawaleta pamoja maqari na mahafidh wa kimataifa wa Qur'ani Tukufu kutoka Iran na nchi zingine za Kiislamu duniani.
Mashindano hayo yanatazamiwa kuendelea hadi Julai sita na maelezo zaidi yatatolewa baadaye.
Mashindano yaliyopita yalifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano mjini Tehran na mwaka huu pia inatazamiwa mashindano hayo yatafanyika katika ukumbi huo.
796826
captcha