Ijumaa iliyopita wafuasi wa chama chenye misimamo ya kufurutu mipaka ya Ataka (yaani hujuma) waliwahujumu Waislamu waliokuwa wakiswali wakati wa sala ya Ijumaa. Kiongozi wa chama hicho Volen Siderov alikuwa akihutubia mkutano karibu na Msikiti wa Banya Bashi mjini Sofia. Kiongozi huyo mwenye chuki dhidi ya raia wa kigeni alisema hawatakubali vipaza sauti vitumike msikitini.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ililaani tukio hilo na kusema kuwa kwa kuzingatia kuwa kuna Waturuki Waislamu karibu laki saba wanaoishi Bulgaria, wakuu wa nchi hiyo wanapaswa kuchukua hatua kali dhidi ya wafuasi wa chama cha Ataka.
798581