IQNA

Mwamko Mashariki ya Kati umesababishwa na ubeberu wa Marekani

15:10 - May 28, 2011
Habari ID: 2129526
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa jijini Tehran Ayatullah Ahmad Khatami amesema leo kuwa mapinduzi na harakati za mageuzi za watu wa Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika zimesababishwa na ubeberu wa Marekani.
Ayatullah Khatami amesema kuwa Marekani imekuwa ikiwakalia wananchi wa maeneo hayo na kuwasukumia madikteta kuwa viongozi wao na kutokana na hilo wananchi wameshindwa kuvumilia na sasa wameamua kuwatimua madarakani vibaraka wa Washington.
Kuhusu yanayoshuhudiwa Bahrain na Yemen, Ayatullah Ahmad Khatami amesema, madikteta wa nchi hizo wanaendelea kuwatendea jinai wananchi wao kila leo kwa ridhaa ya Marekani pasina kuona haya. Amesema utawala wa kiimla wa Aal Khalifa huko Bahrain umekwenda mbali na kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu kwa kuchoma misikiti kwa Amri ya Marekani.
Ayatullah Ahmad Khatami ametoa wito kwa Waislamu duniani kuwaunga mkono wananchi wa Bahrain na kulaani jinai wanazofanyiwa Waislamu wa Bahrain na utawala katili wa Aal Khalifa.
799154
captcha