Kituo cha upashaji habari cha Ahlulquran kimeripoti kuwa mashindano hayo yatafanyika kipindi cha joto kali mwakani yakisimamiwa na akademia hiyo katika mji wa Tampa huko magharibi mwa jimbo la Florida.
Akademia ya Ahlulquran imetangaza kuwa watu wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanapaswa kuwa wamejiandikisha hadi kufikia tarehe 20 Mchi 2012. Mashindano hayo yanajumuisha hifdhi ya Qur'ani nzima kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 23, kuhifadhi suratul Baqarah au Aal Imran kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 21, kuhifadhi suratu Nisa au Maida kwa wenye umri wa miaka chini ya 21, kuhifadhi sura ya Hud au Yusuf kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 21, kuhifadhi suratu Raad au Ibrahim kwa wenye umri wa chini ya miaka 18 kuhifadi juzuu ya 25 au 26 kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 18, kuhifadhi suratu Qaf au Najm kwa wenye umri wa chini ya miaka 16 na kuhifadhi juzuu ya 27 au 28 au 29 makhsusi kwa watu wenye umri wa chini ya miaa 16.
Watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka 12 pia watashiriki katika mashindano ya kuhifadhi juzuu ya 30 ya Qur'ani Tukufu, hifdhi ya nusu ya juzuu ya 30 kwa wenye umri wa chini ya miaka 8 na hifdhi ya robo ya juzuu Amma kwa wenye umri wa chini ya miaka 6.
Akademia ya Qur'ani ilianzishwa mwaka 1998 katika mji wa Tampa, Florida kwa shabaha ya kuhamasisha Waislamu kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kuzingatia aya zake. Akademia hiyo husimamia mashindano na programu mbalimbali za masomo ya Qur'ani kila mwaka. 800298