Akizungumza na IQNA, amesema kozi hizo zitafanyika katika msimu wa joto mwaka huu na kuongozwa na wataalamu wa kimataifa wa Qur’ani Tukufu.
Amesema kati ya kozi zitakazofunzwa mwaka huu ni Tajweed (kiwango cha msingi na thanawi), qiraa (sauti na lahani), hifdhi (kwa watoto na watu wazima), tafsiri ya Qur’ani, tarjumi na tafsiri ya Nahjul Balagha.
Ameongeza kuwa kozi za Qur’ani zilizofunzwa katika msimu wa machipuo mjini Tehran zilipokelewa vizuri na wananchi wapendao Qur’ani.
800320