IQNA

Kituo cha Utamaduni cha Qur’ani Tehran kutoa mafunzo maalumu ya sayansi za Qur’ani

9:39 - May 30, 2011
Habari ID: 2130471
Kituo cha Utamaduni cha Qur’ani mjini Tehran katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kinatoa kozi maalumu za sayansi za Qur’ani, amesema mkurugenzi wa kituo hicho Leyli Akbarpour.
Akizungumza na IQNA, amesema kozi hizo zitafanyika katika msimu wa joto mwaka huu na kuongozwa na wataalamu wa kimataifa wa Qur’ani Tukufu.
Amesema kati ya kozi zitakazofunzwa mwaka huu ni Tajweed (kiwango cha msingi na thanawi), qiraa (sauti na lahani), hifdhi (kwa watoto na watu wazima), tafsiri ya Qur’ani, tarjumi na tafsiri ya Nahjul Balagha.
Ameongeza kuwa kozi za Qur’ani zilizofunzwa katika msimu wa machipuo mjini Tehran zilipokelewa vizuri na wananchi wapendao Qur’ani.
800320
captcha