Kwa mujibu wa tovuti ya al-Wafd ya Misri, muungano huo umeyataka mashirika na jumuiya za kijami na za serikali katika nchi za Kiarabu na za Magharibi kushirikiana na wananchi katika kufanikisha maandamano hayo ya kuwaunga mkono watu wa Bahrain wanaopambana na watawala dhalimu wa kifalme nchini humo. Maandamano hayo yanatazamiwa kufanyika mbele ya balozi za Bahrain katika miji mikuu ya Cairo Misri, London Uingereza, New York Marekani, Baghdad Iraq, Beirut Lebanon, Nouakchott Mauritania na Algiers nchini Algeria.
Muungano huo pia umeyataka mataifa ya Kiarabu kushirikiana na mashirika ya habari na ya kupigania haki za binadamu duniani ili kuyaakisi vyema maandamano hayo katika upeo wa kimataifa na kudhihirisha sura halisi ya ukandamizaji wa watawala hao dhidi ya raia wasio na hatia.
Wakati huohuo Wabahrain wanapanga kufanya maandamano makubwa hapo siku ya Ijumaa tarehe Tatu Juni ili kusisitiza juu ya utekelezwaji wa haki zao za kimsingi. 800921