IQNA

Hatua za makundi ya chuki dhidi ya Uislamu zachunguzwa ufaransa

13:30 - May 31, 2011
Habari ID: 2131519
Hatua za makundi yenye chuki na misimamo ya kupindukia mipaka dhidi ya Uislamu zilichunguzwa jana Jumatatu tarehe 30 Mei kupitia kanali ya televisheni ya nchi hiyo ya CANAL+.
Suala la chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya na sababu za kuenea kwake na malengo ya makundi ya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu ni mambo yaliyochunguzwa na kujadiliwa kwenye kipindi hicho cha televisheni.
Kipindi hicho pia kimejadili nafasi ya Geert Wilders, mtengeneza filamu inayovunjia heshima matukufu ya Kiislamu kwa jina la Fitna na makundi mengine yaliyo na misimamo ya chuki dhidi ya Uislamu nchini Uswisi katika kueneza hofu na wasiwasi dhidi ya Uslamu katika nchi za Magharibi.
Mwishoni mwa kipindi hicho cha televisheni makundi hayo yenye misimamo ya kupindukia mipaka yametajwa kuwa ya hadaa na ujanja. Washiriki wa kipindi hicho wamesema kuwa makundi hayo yanaeneza chuki na uongo dhidi Uislamu ili kufunika matatizo ya kiuchumi na kijamii yanayozitatiza nchi nyingi za Magharibi, na hivyo kuthibitisha wazi kutofaa kwao mbele ya fikra za waliowengi duniani. 801524
captcha