Ali Akbar Salehi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amepinga kutatuliwa migogoro ya eneo la Mashariki ya Kati kwa kutumia njia za kijeshi na kuzilaumu baadhi ya nchi za eneo hili kwa kutuma wanajeshi wao huko Bahrain, akisema kuwa hatua hiyo itashadidisha zaidi migogoro hiyo.
Akihutubia katika mkutano wa Mwamko wa Kiislamu hapa mjini Tehran, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema uingiliaji kijeshi unaofanywa na nchi kadhaa za kigeni huko Bahrain umeubadili mgogoro wa ndani wa nchi hiyo na kuufanya wa kieneo na kimataifa na kwamba hatua kama hizo haziwezi kuhalalishwa. Amesema Iran inapinga uingiliaji wowote wa kigeni na ukaliaji wa mabavu unaofanywa na nchi nyingine huko Bahrain na Libya na kuongeza kuwa uingiliaji kijeshi wa aina hiyo ni tishio kuu kwa amani na usalama wa eneo.
801934