IQNA

Mkutano wa Kimataifa wa Maulamaa wa Kiislamu waanza Senegal

14:32 - June 06, 2011
Habari ID: 2133692
Mkutano wa Kimataifa wa Maulamaa wa Kiislamu umeanza Jumatatu hii huko Dakar mji mkuu wa Senegal.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mkutano huo umeanza saa nne asubuhi kwa saa za Dakar. Hotuba ya ufunguzi imetolewa na Rais Abduolaye Wade wa nchi hiyo ambaye amezungumza kuhusu nafasi ya maulamaa wa Kiislamu katika matukio ya dunia.
Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na Rais wa Senegal ambaye pia ni mMwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC.
Maulamaa wa Kiislamu na wasomi kutoka nchi zote za Kiislamu wanahudhuria mkutano huo kwa lengo la kujadili matukio ya kieneo na kimataifa.
803598
captcha