IQNA

'Hadithi za Wanyama katika Qu'rani' kuchapishwa

14:25 - June 06, 2011
Habari ID: 2133707
Kitabu chenye anwani ya 'Hadithi za Wanyama katika Qu'rani' kilichoandikwa na mwandishi wa Lebanon Ahmad Bahjat kitazinduliwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran.
Haya ni kwa mujibu wa Hamid Reza Seyyed Naseri mkuu wa Shirika la Uchapishaji la Zekr. Amesema juzuu 5 za kitabu hicho zitazinduliwa katika maonyesho hayo ya Qur'ani ambayo yatafanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili ya watoto na vijana na kinajumuisha hadithi tano za wanyama katika Qur'ani ambapo kuna kisa cha Hud Hud na Nabii Suleiman AS, kisha cha Nyangumi na Nabii Yunus AS, kisa cha Ngamia na Nabii Saleh na vile vile kisa cha Kunguru na Habil na Kabil na Ndovu katika jeshi la Abraha.

801922
captcha