IQNA

Mahakama ya Kenya kusikiliza kesi ya hijab

13:47 - June 07, 2011
Habari ID: 2134106
Kesi iliyowasilishwa na mwanafunzi wa kike Muislamu dhidi ya shule moja nchini Kenya akitaka aruhusiwe kuvaa hijab shuleni itaanza kusikilizwa Juni 14.
Binti huyo, kupitia mama yake, alifungua kesi dhidi ya Shule ya Sekondari ya Kenya High mwaka 2010 akitaka shule hiyo ishurutishwe kuwaruhusu wanafunzi wa kike wavae hijabu ambayo ni wajibu kwa wanawake Waislamu. Binti huyo anasema kuwa shule hiyo inakiuka sheria kwa kukataa kutekeleza amri iliyotolewa na Wizara ya Elimu ya Kenya ambayo Julai mwaka 2010 iliamuru shule zote nchini humo kuwarushusu wasichana/wanawake Waislamu kuvaa hijabu shuleni.
Uongozi wa shule hiyo ulikataa kufika mahakamani May 30 wakati wa kusikilizwa kesi hiyo na hivyo kupelekea kuakhirishwa kwake. Jaji anayesikiliza kesi hiyo ameionya shule hiyo kuwa itachukuliwa hatua kali iwapo haitafika mahakamani Juni 14.
Baadhi ya shule nchini Kenya zina waalimu wenye misimamo mikali ya Kikristo ambao wanawanyima wanafunzi Waislamu haki ya kvuaa vazi na staha la mwanamke wa Kiislamu hijabu katika hali ambayo serikali ya nchi hiyo imeidhinisha uvaliwaji hijabu shuleni.
804180
captcha