IQNA

Chuo cha Kiislamu cha Malaysia kuzinduliwa

13:51 - June 07, 2011
Habari ID: 2134215
Chuo cha Kiislamu cha Malaysia kitazinduliwa hivi karibuni chini ya usimamizi wa Taasisi ya Ustawi ya Kiislamu ya nchi hiyo (JAKIM).
Kwa mujibu wa shirika la habari la Malaysia Bernama, habari hiyo imetolewa na Jamil Kheir Habram, Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Malaysia na kuongeza kuwa chuo hicho kitaanzisha shughuli zake kwa muda katika Chuo cha Kimataifa cha Kiislamu cha Malaysia (UIAM).
Habram amesema chuo hicho kitaendeshea shughuli zake katika majengo ya chuo cha UIAM hadi taasisi iliyotajwa ya ustawi itakapotenga sehemu maalumu ya kuendeshewa shughuli za kudumu za chuo hicho na taasisi nyingine zitakazobuniwa chini yake.
Amesema shughuli za chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 1955 zilisimamishwa kwa muda mwaka 1970 kutokana na sababu zisizoepukika.
Chuo hicho kitaanzisha tena shughuli zake katika fremu ya mipango ya kielimu ya serikali ya Malaysia ya kuimarisha elimu ya juu ya Kiislamu nchini. 804126
captcha