IQNA

Wazayuni wateketeza moto msikiti katika Ukingo wa Magharibi

14:10 - June 07, 2011
Habari ID: 2134216
Walowezi wa Kizayuni leo alfajiri wameshambulia na kuteketeza moto msikiti mmoja katika kijiji cha al-Mughayyir karibu na mji wa Ramallah ulioko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Kwa mujibu wa gazeti la Quds al-Arabi linalochapishwa Palestina, Jihad an-Nuusan mmoja wa wanamapambano ya Kiislamu na mkazi wa kijiji kilichotajwa amesema kwamba wakazi wa kijiji hicho waliona ndimi za moto na moshi ukitokea kwenye madirisha ya msikiti huo. Hata hivyo wanakijiji walifanikiwa kuuzima moto huo kabla ya kuenea katika sehemu nyingine za msikiti huo.
An-Nuusan ameeongeza kuwa walowezi wa Kizayuni waliuzungushia msikiti huo matairi ya magari kwa lengo la kuuteketeza wote lakini wanakijiji walifanikiwa kuondoa baadhi ya matairi hayo kabla ya kushika moto. Amesema kwa kutilia maanani kwamba Wazayuni ndio wanaodhibiti usalama wa kijiji hicho ni wazi kuwa wao ndio wanaowajibika kulinda usalama wa kila eneo takatifu na kila mwananchi anayeishi katika kijiji hicho.
Vilevile wakazi wa kijiji hicho wameona maandishi ya kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu yaliyoandikwa na Wazayuni kwa lugha ya Kiibrania kwenye milango na kuta za msikiti huo. 804410
captcha