IQNA

Wiki ya Imam Khomeini yaadhimishwa Nigeria

14:38 - June 08, 2011
Habari ID: 2134905
Waislamu nchini Nigeria wamejiunga na Waislamu wenzao kote duniani katika kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa 22 wa kuaga dunia Imam Khomeini (S) ambapo kumefanyika hafla mbalimbali katika 'Wiki ya Imam Khomeini'.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria na yalianza tarehe 2 hadi 4 Juni.
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaki alitoa hotuba iliyokuwa na anwani ya 'Imam Khomeini na Fikra ya Utawala wa Faqihi (Wilayatul Faqih)
Amesema itikadi ya Wilayatul Faqih haikuanzishwa na Imam Khomeini bali shakhsia huyo aliihuisha.
Naye mwanaharakati wa Kiislamu Bi Malama Zeenat Ibrahim alitoa hotuba kuhusu maisha ya Imam Khomeini.
Aidha aliashiria ustawi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa ulimwengu unapaswa kufuata mafundisho ya Imam Khomeini.
Amesema Imam Khomeini alileta mwamko wa Kiislamu miongoni mwa Waislamu duniani kufuatia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Ametoa wito kwa Waislamu kufuata mafundisho ya Imam Khomeini.
Vilevile 'Wiki ya Imam Khomeini ilijumuisha maonyesho ya vitabu na picha zinazohusu Imam Khomeini na mapinduzi ya Kiislamu.
805030
captcha