IQNA

Mpango maalumu wa kuhifadhi Qur’ani kuanza Qatar

14:55 - June 08, 2011
Habari ID: 2134952
Mpango wa kina wa kuhifadhi Qur’ani Tukufu unatazamiwa kuanza Qatari kuanzia tarehe 17 Julai.
Kwa mujibu wa gazeti la Ash-Sharq, mpango huo ujulikanao kama Quras umeandaliwa na kitengo cha wanawake cha Idara ya Kuhifadhi Qur’ani cha Taasisi ya Misaada ya Ash Sheikh Eid.
Mkurugenzi wa idara hiyo amesema mpango huo ni maalumu kwa wanawake na kila anayetaka kushiriki ni sharti awe amehifadhi kwa uchache juzuu mbili za Qur’ani.
Lengo la mashindano hayo limetajwa kuwa ni kustawisha kiwango cha kuhifadhi Qur’ani miongoni mwa wanawake na kuwahimiza kuendeleza harakati za kuhifadhi Qur’ani.
803811
captcha