IQNA

Wasiwasi watanda Uingereza kuhusu kushadidi ubaguzi dhidi ya Waislamu

19:05 - June 08, 2011
Habari ID: 2135158
Baraza la Waislamu wa Briteni (Britain) (MCB) lilitangaza katika taarifa iliyotolewa jana kwamba lina wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la ubaguzi dhidi ya Waislamu nchini Uingereza.
Baraza hilo limesema kuwa lengo la juhudi zinazofanywa na serikali kwa ajili ya kubuni sheria mpya eti za kupambana na misimamo mikali ni kuwabana zaidi Waislamu.
Sehemu moja ya taarifa ya MCB imesema: "Kupasisha sheria zinazochafua jina la Waislamu na kufungamanisha Uislamu na vitendo vya kigaidi hakutasaidia juhudi za kupunguza ugaidi duniani, na siasa zinazotekelezwa sasa na serikali ya David Cameron ni mwendelezo wa siasa zilizokuwa zikitekelezwa nchini Uingereza baada ya matukio ya Septemba 11.
Mwishoni mwa taarifa hiyo Baraza la Waislamu wa Briteni limeashiria kuwa siasa zinazotekelezwa na serikali ya London zina upendeleo na kusema kuwa tokea sasa baadhi ya makundi na jumuiya za Kiislamu zimeorodheshwa katika listi ya makundi yenye misimamo mikali na serikali imesimamisha misaada yake ya kifedha kwa taasisi na makundi hayo." 805345

captcha