IQNA

Kikao cha kimataifa cha Mashirika ya Masuala ya Kibinadamu chafunguliwa Sudan

19:46 - June 08, 2011
Habari ID: 2135162
Kikao cha nne cha kimataifa cha Mashirika ya Masuala ya Kibinadamu ya Nchi za Kiislamu kimefunguliwa leo Jumatano huko Khartoum, mji mkuu wa Sudan.
Kikao hicho cha siku moja ambacho kimefunguliwa na Rais Omar Hassan al-Bashir kimeandaliwa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Uhubiri wa Kiislamu ya Sudan chini ya anwani ya 'Mashirika ya Jamii ya Kiraia; Majukumu na Nafasi.'
Ekmeleddi Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC, Abdallah Badawi, Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia na wawakilishi wa zaidi ya mashirika ya kieneo na kimataifa yapatayo 100 ni miongoni mwa shakhsia wanaoshiriki katika kikao cha leo huko Sudan.
Akizungumzia juu ya umuhimu wa kikao hicho, Sawar ad-Dhahb, mkuu wa Taasisi ya Uhubiri wa Kiislamu ya Sudan amesema kikao hicho kina umuhimu maradufu hasa katika mazingira ya hivi sasa ambapo nchi za Kiislamu zinakabiliwa na changamoto kubwa, njama za maadui na jamii za Waislamu waliowachache kukumbwa na vitisho tofauti. Amesema vitendo vya ugaidi vinatishia ulimwengu wa Kiislamu na kwamba kutuhumiwa Waislamu kwamba wanahusika na viendo vya ugaidi kumevuruga sana juhudi za kuhubiri na kueneza Uislamu katika nchi za Magharibi.
Sawar ad-Dhahb amesema serikali ya Sudan itanufaika na kikao hicho katika kuyashawishi mashirika ya misaada ya kibinadamu ya nchi za Kiislamu yawafikishie misaada ya dharura wananchi wanaohitajia misaada wa nchi hiyo na hasa wale wa eneo linalokumbwa na mgogoro wa ndani la Darfur. 805430
captcha