IQNA

Mpango wa Intaneti wa kupambana na chuki dhidi ya Uislamu

13:30 - June 09, 2011
Habari ID: 2135291
Mpango wa Intaneti unaoitwa 'Mwananchi Mwenzangu wa Marekani' umeanzishwa na Taasisi ya Umoja ya Upashaji Habari UPF kwa madhumuni ya kupambana na tatizo la chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Islam Today taasisi hiyo iliyoanzishwa nchini Marekani mwaka 1999 hujishughulisha na uzalishaji wa filamu za matukio ya kweli kwa ajili ya kuwashawishi wafuasi wa dini tofauti waishi pamoja kwa amani.
Katika mpango huo wafuasi wa dini hizo wametakiwa wasimame imara na kukabiliana na mielekeo ya chuki dhidi ya Uislamu ambayo katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikienea kwa kasi kubwa nchini humo. Watazamaji wasiokuwa Waislamu ambao wanatazama filamu fupi ambazo zimetayarishwa kupitia mpango huo wanatakiwa wawasilishe maoni yao mazuri kuhusiana na jinsi walivyojuana na Waislamu ambao wana uhusiano nao. Kufikia sasa Wamarekani wengi wameshawasilisha maoni yao kuhusiana na jambo hilo.
Watayarishaji wa mpango huo wanasema kuwa lengo lao ni kutolewa majibu mazuri na ya kuridhisha kwa wale wanaoeneza chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. 805485
captcha