IQNA

Dakta Larijani:

Teknolojia ya nyuklia ya Iran ni ya Waislamu wote

13:48 - June 11, 2011
Habari ID: 2135601
Dakta Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani bunge amesema kuwa, teknolojia ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani ni kwa ajili ya mataifa yote ya Kiislamu ulimwenguni.
Akizungumza kwenye kongamano lililofanyika jana katika Chuo Kikuu cha Hidayatullah mjini Jakarta nchini Indonesia, Spika Larijani ameongeza kuwa, nchi za Kiislamu zina uwezo mkubwa wa kiuchumi na kwa sababu hiyo ndiyo maana Iran inataka kushirikiana na nchi zote za Kiislamu na hasa serikali ya Indonesia. Huku akisisitiza kwamba nchi za Kiislamu zinapaswa kuwa na uwezo wa kujilinda, Dakta Larijani ameongeza kuwa, Iran imepanga mikakati ya kuwa na mifumo ya makombora ya kisasa kwa ajili ya kujihami yenyewe pamoja na kuzihami nchi nyingine za Kiislamu.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima iko bega kwa bega na nchi zote za Kiislamu na pindi Marekani na Wazayuni watakapojaribu kufanya harakati chafu dhidi ya nchi za Kiislamu, nchi hizo zitakabiliwa na upinzani mkali wa Iran, amesisitiza larijani. Indonesia inahesabiwa kuwa ni nchi inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya Waislamu duniani.
805896
captcha