Msemaji wa ICC amesema darsa hizo ni wazi kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu ambao wanataka kuufahamu vyema zaidi ujumbe wa Qur’ani. Amesema lengo la Kituo cha Maelezo ya Kiislamu ni kueneza msingi wa Qur’ani Tukufu wa ‘Iqra’ yaani kusoma kwa wote. Amesema ujuzi na maarifa ndio msingi wa hekima.
Amesema Darsa za Sayansi za Qur’ani zitaangazia aliyoteremshiwa Mtume wa Mtukufu Uislamu.
Taasisi hiyo ya Malaysia inalenga kueneza mafundisho ya Qur’ani Tukufu kwa wanadamu wote kwani ujumbe wa Qur’ani haukuteremshwa tu kwa Waislamu bali umewahutubu pia wanadamu wa dini mbalimbali.
805993