Kituo cha habari cha Ic-el kimeripoti kuwa katika masomo hayo ambayo yanasimamiwa na kitengo cha lugha ya Kiingereza cha Kituo cha Kiislamu cha Uingereza, Waislamu wapya wanajifunza Qur’ani katika awamu tatu za utangulizi, masomo ya kati na masomo ya juu.
Katika masomo ya utangulizi, Waislamu hao wapya wanajifunza lugha ya Kiarabu na kusoma Qur’ani na katika awamu nyingine wanapewa mafunzo ya sheria za tajwidi na Qur’ani Tukufu.
Masomo hayo yanatolewa kila wiki siku za Jumamosi kuanzia saa 11 hadi saa moja jioni kwa wakati wa Uingereza. Kila kikao kitajumuisha masomo ya Qur’ani, sheria za Kiislamu na mjadala kuhusu uhuru. 806553