Marc George, mwanachama wa zamani wa Baraza Kuu la Chama cha Kitaifa cha Ufaransa, baada ya miaka mingi ya kufanya njama na harakati za kisiasa na kiuadui dhidi ya Uislamu hatimaye ametangaza rasmi kusilimu na kukubali mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa tovuti ya chretiente Marc George Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Udugu na Umoja wa Kitaifa ya Ufaransa ambaye pia ni Mkurugenzi wa tovuti ya www.medialibre.eu ametangaza kupitia taarifa katika tovuti hiyo kwamba amesilimu na kuukubali Uislamu.
Baada ya kuwa mwanachama wa miaka mingi wa chama kilichotajwa cha Ufaransa ambacho ni chama kilicho na misimamo mikali na ya kupindukia dhidi ya Uislamu, amejiondoa kwenye chama hicho na kuanzisha tovuti ya www.medialibre.eu, tovuti ambayo inafuatilia kwa karibu matukio muhimu ya dunia na hasa ya Palestina. Shughuli za Marc George kuhusiana na matukio ya ulimwengu wa Kiislamu zimempelekea kuufahamu vyema Uislamu na hatimaye kuukubali. 806966