IQNA

Iran kuandaa kikao cha kimataifa dhidi ya ugaidi

14:57 - June 13, 2011
Habari ID: 2137049
Iran inaandaa kikao cha kimataifa cha kupambana na ugaidi ambacho kitahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 80 pamoja na taasisi za kieneo na kimataifa.
Kikao hicho kitafanyika Juni 25-26 kwa lengo la kuimarisha mshikamano wa kimataifa katika kupambana na ugaidi chini ya kaulimbiu ya 'Dunia Bila Ugaidi'.
Kwa mujibu wa Mohammad Hassan Saleh Maram ambaye ni Naibu Mkuu wa Idara ya Mawasiliano katika Ofisi ya Rais wa Iran, kati ya mada zitakazojadiliwa katika kongamano hilo la siku mbili ni mbinu za kupambana na ugaidi.
Maram amesema Iran imezindua mtandao wa intaneti katika www.icterrorism.com ambao una mitazamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu vita dhidi ya ugaidi.
807071
captcha