Blair amekuwa akizungumza kuhusu umuhimu wa dini tokea aondoke Ikulu ya Downing Street mjini London mwaka 2007. Kwa mujibu wa Tovuti ya Islamonline, Blair aliyekuwa akifuata madhehebu rasmi ya kikristo ya Uingereza ya Protestanti alibadilisha na kuanza kufuata Ukatoliki baada ya kuondoka madarakani.
'Nasoma Qur'ani kila siku. Moja ya sababu ni kufahamu yanayojiri duniani lakini sababu kuu ni kuwa kitabu hiki kina miongozo ya kina'.
Blair amesema ufahamu wa kina wa imani unamsaidia kama mjumbe maalumu wa Mashiriki ya Kati wa kundi la pande nne zinazosimamia mpango wa amani ya Mashariki ya Kati wa Road Map linalojumuisha Umoja wa Mataifa, Marekani, Umoja wa Ulaya na Russia.
Kusoma Qur'ani pia kunamkutanisha Blair pamoja na shemeji yake Bi. Lauren Booth. Dada huyo wa Cherie, mke wa Blair, alisilimu mwaka jana baada ya kile alichokitaja kuwa ni 'tajruba ya kimaanawi' alipokuwa akitembelea Haram Takatifu ya Bibi Fatima Maasuma SA katika mji wa Qum katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
808067