Duru ya tisa ya kimataifa ya masomo ya hifdhi ya Qur'ani ya kipindi cha kiangazi itaanza katika Mskiti wa al Hamraa katika mji wa Dammam, Saudi Arabia kwa kuwashirikisha watu kutoka mikoa mbalimbali ya nchi hiyo na nchi nyingine za Ghuba ya Uajemi.
Duru hii ya mafunzo ya Qur'ani inasimamiwa na idara ya Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya eneo la mashariki mwa Saudi Arabia chini ya uongozi wa Wizara ya Wakfu ya nchi hiyo.
Kiongozi wa duru hiyo ya hifhi ya Qur'ani ya kimataifa Khalid Abdullah Aal Said amesema kazi ya kuandikisha majina ya washiriki katika masomo hayo itaanza kesho Alkhamisi kupitia mtandao wa intaneti wa www.hamraq.net na kuendea kwa siku tatu.
Wanafunzi na wasokuwa wanafunzi, raia wa Saudia na raia wa kigeni wanaoishi nchini humo wanaopendelea masuala ya Qur'ani kutoka nchi za Ghuba ya Uajemi wanaruhusiwa kushiriki katika masomo hayo.
Amesema kuwa maulamaa wa kidini na shakhsia wa kisiasa na kiutamaduni wa Saudia watakagua shughuli hizo za masomo ya Qur'ani.
Khalid Abdullah amesisitiza kuwa tarehe ya kufanyika duru hiyo ya masomo ya hifdhi ya Qur'ani itatangazwa baadaye. 809227