IQNA

Iran kuajiri walimu 5000 wapya wa Qur’ani

12:45 - June 18, 2011
Habari ID: 2139698
Wizara ya Elimu ya Iran imetangaza kwamba inapanga kuajiri walimu 5000 wapya ili kuinua kiwango cha masomo ya Qur’ani katika shule nchini.
Naibu Waziri wa Elimu Zakaria Yazarlu amesema wizara hiyo inahitajia walimu zaidi wa Qur'ani na kuongeza kuwa mpango huo unatazamiwa kuidhinishwa na Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani bunge la Iran na serikali.
Ameongeza kuwa madrasa maalumu za Qur’ani nchini Iran sasa ni 10,000 na idadi hiyo inatazamiwa kufika 20,000 katika mustakabali wa karibu. Amesema sambamba na kuongezeka idadi ya madrasa za Qur’ani nchini vilevile kiwango cha elimu katika vyuo hiyo kitaongezeka.


809464
captcha