IQNA

Kuunga mkono mwamko wa Bahrain ni wajibu wa kidini

12:50 - June 18, 2011
Habari ID: 2139708
Baraza la Maulamaa wa Kishia wa Bahrain limesema kuunga mkono mwamko wa wananchi wa nchi hiyo ni wajibu wa kidini.
Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa Juni 17, baraza hilo limesisitiza kuwa litasimama bega kwa bega na wananchi wanamapinduzi wa Bahrain katika kupigania haki zao za kisheria.
‘Ingawa baraza hili ni taasisi ya kidini na wala si ya kisiasa lakini halitapuuza ukweli kuhusu hali ya sasa ya kisiasa na mwamko wa wananchi hapa nchini’.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa hatua ya baadhi ya makundi potofu kuhujumu itikadi na thamani za maulamaa wa Bahrain ni njama ya kuharibu sura ya wanazuoni hao na kuvunja imani waliyonayo watu kwa wanazuoni wa Kishia.
Baraza la Maulamaa wa Kishia Bahrain limesisitiza kuwa matakwa ya wananchi wa Bahrain ni ya Kiislamu na wala hayahusu masuala ya kimadhehebu.
809994
captcha