Akizungumza Jumamosi mjini Tehran, Rais Ahmadinejad amesema nadharia hiyo ya ubepari hatimaye itapelekea kuangamizwa mazingira.
Amesema tamaa isiyo na mwisho na kujitakia makuu katika baadhi ya nchi ndio tishio kubwa kwa mazingira. Rais wa Iran amesema kuwa ili kujaza mifuko wa mabepari mafisadi walio dhidi ya ubinadamu, madola ya kibeberu yamevuruga uhusiano wote wa mwanadamu ukiwemo na mazingira. Rais Ahmadinejad amesema wale walioanzisha biashara ya utumwa ndio waliohujumu na kuyakoloni mataifa mengine na sasa wanalenga kuharibu mazingira kupitia sera zao za kibepari. Rais wa Iran amesema ni jukumu la kila mwanadamu kulinda mazingira.
810699