Akizungumzia suala hilo Ekmeleddin Ihsanoglu Katika Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC amekaribisha uanachama wa nchi hiyo katika jumuiya ya OIC na pia kumkaribisha Muhammad Shaukat kuwa mwakilishi maalumu wa Uingereza katika jumuiya hiyo ambayo ni mjumuiko mkubwa zaidi wa nchi za Kiislamu duniani.
Baada ya kukubaliwa uanachama wa Uingereza katika jumuiya ya OIC Ihsanoglu amefanya safari ya siku nne nchini humo kwa lengo la kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo akiwemo David Cameron Waziri Mkuu na William Hague Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kuhusiana na haja ya kuimarishwa ushirikiano na uhusiano wa pande mbili. Ihsanoghlou vilevile amekutana na kuzungumza na viongozi wa jamii ya Kiislamu nchini Uingereza na kujadili shughuli za jamii hiyo nchini humo.
Nchi wanachama watazamaji katika jumuiya ya OIC wanaweza kushiriki kwenye vikao vyote vya jumuiya hiyo lakini hazina haki ya kupiga kura wala kuwasilisha mswaada wa azimio lolote katika jumuiya hiyo.
Baadhi ya nchi zimejiunga na jumuiya hiyo kwa madhumu ya kulinda haki za jamii za Waislamu waliowachache wanaoishi katika nchi hizo. Mbali na Uingereza nchi nyingine nane zikiwemo za Belarus, Afrika Kusini, Ufilipino, Sri Lanka, Serbia na Nepal pia zimeomba kujiunga na jumuiya ya OIC kama wanachama watazamaji. 810539