Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Mohammadi akihutubia waandishi habari Jumapili mjini Tehran amesema duru ya 28 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni moja kati ya matukio muhimu zaidi duniani. Amesema mashindano hayo yatakuwa na vitengo vya hifdhi na qiraa na yatafanyika mjini Tehran tarehe 27 Rajab kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kubaathiwa Mtume SAW.
Amesema kitengo cha makala katika mashindano hayo kitaangazia zaidi suala la mwamko wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.
Mashindano hayo yanatazamiwa kufunguliwa rasmi na Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran nazo sherehe za kufunga mashindano zitaongozwa na Ayatullah Amoli Larijani Mkuu wa Vyombo vya Mahakama hapa nchini.
811155