Gazeti la al Bilad la Saudi Arabia ambalo halikutaja tarehe maalumu ya siku ya mashindano hayo limeripoti kuwa sherehe ya kufunga mashindano hayo itahudhuriwa na Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Saudia Saleh bin Abdulaziz Aal Sheikh na Rais wa Indonesia.
Mashindano hayo ya kuhifadhi Qur’ani na Hadithi yanapewa umuhimu mkubwa na Rais wa Indonesia na wawakilishi wa nchi wanachama katika jumuiya ya Asean.
Wakati huo huo mashindano ya kitaifa ya Qur’ani ya Indonesia yanaendelea yakiwashirikisha wasomaji 186 kutoka miji 55 ya nchi hiyo. 811885