Kozi hiyo ya wiki 16 iliyokuwa na anwani ya ‘Kozi ya Sheria za Kiislamu kwa Majaji na Waendesha Mashtaka’ iliwashirikisha wataalamu 12 wakiwemo majaji na waendesha mashtaka kutoka maeneo yote ya Pakistan.
Akizungumza katika hafla hiyo Rais wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu cha Islamabad Dr. Mumtaz Ahmad amewapongeza washiriki kwa kufuzu katika kozi hiyo. Amesema Wapakistani wote wanatumai kuwa vyombo vya mahakama nchini humo vitafanya kazi bila kuathiriwa na mashinikizo.
812547