Katika masomo hayo washiriki watajifunza hifdhi ya Qur’ani Tukufu, adhan, upigaji picha na mbinu za kusoma.
Mashindano ya Qur’ani yatakuwa katika makundi mawili moja la washiriki walio na umri wa miaka 7-13 na la pili kwa walio na umri wa miaka 14-18. Aidha kutakuwa na programu maalumu kwa ajili ya wasichana.
Wataalamu kutoka Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Imarati watawasaidia watoto kufahamu sheria za kusoma Qur’ani Tukufu.
Talal al Mazroui Mkurugenzi wa Mipango katika msikiti huo amesema kuna mikakati ya kutoa mafunzo kwa kizazi cha vijana kuhusu thamani na mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu. 812517