Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu katika ukumbi wa Taasisi ya Sayansi za Kiislamu mjini Muscat, al Riyami ametangaza matokeo ya vitengo vitano ya hifdhi kamili na sehemu ya Qur’ani Tukufu. Amesema washiriki wa mashindano hayo yaliyoanza Machi ni 614 katika vituo 17. Amesema mashindano ya mchujo yalianza Aprili 9 ambapo washiriki 177 walifuzu kuingia katika fainali iliyoanza Aprili 23, ambapo 146 walifanikiwa. Amesema mashindano ya 22 yatafanyika mwaka 2013. 812462