IQNA

Maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya vitabu katika Ukanda wa Gaza

14:33 - June 22, 2011
Habari ID: 2142426
Wizara ya Utamaduni ya serikali ya Hamas katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa maonyesho ya kwanza ya kimataifa yamepangwa kufanyika katika Ukanda huo kati ya tarehe 5 hadi 23 mwezi Oktoba kwa ushirikiano wa wachapishaji na wasambazaji wa vitabu wa nchi za Kiarabu.
Akizungumzia suala hilo Mustafa as-Swawwaf, Mshauri wa Waziri wa Utamaduni wa Hamas amesema kwamba mashauriano makubwa yamekuwa yakiendelea kati ya wizara hiyo na wachapishwaji kwa madhumuni ya kufanikisha maonyesho hayo ya kwanza. Amesema Muungano wa Wasambazaji Vitabu wa Kiarabu utashiriki kwenye maonyesho hayo kwa madhumuni ya kuvunja mzingiro na mbano wa kiutamaduni unotekelezwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina wanaoishi katika ukanda huo.
Amesema huo utakuwa ni mwanzo wa kuvunjwa mzingiro huo wa kiutamaduni na kiuchumi ambao umekuwa ukitekelezwa dhidi ya Wapalestina kwa muda wa miaka mitano sasa.
Mustafa as-Swawwaf, amesema, uimarishaji wa utamaduni wa Kiislamu na Kiarabu wa wakazi wa Gaza kwa madhumuni ya kukabiliana na hujuma ya kiutamaduni ya Wazayuni wa Israel na nchi za Magharibi ni lengo jingine la kufanyika maonyesho hayo ya kimataifa. 812481
captcha